Taarifa kutoka TFF naambiwa mashabiki wa mpira wa miguu nchini watapata nafasi ya kushushuhudia bure mechi ya timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake yaani Twiga Stars na ile ya Zambia ya Shepolopolo.
Mechi hii itakua ya marudiano ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC)ambayo itachezwa Ijumaa ya Februari 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi 88.5 Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili alasiri.
Twiga Stars ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Lusaka ambayo ilikua Februari 14 mwaka huu kwa mabao 2-1 kwa sasa iko kambini chini ya Kocha Rogasian Kaijage na msaidizi wake Nasra Juma ikijiwinda kuwakabili Wazambia wanaotarajiwa kuingia nchini Februari 26 mwaka huu.