Jumamosi ya August 12 2017 ni siku ya kihistoria kwa soka la Tanzania, kwani kesho ndio siku ambayo tutamjua Rais mpya wa shirikisho la soka Tanzania TFF baada ya wajumbe kupiga kura na kumchagua mjini Dodoma.
Wanaogombea Urais ni Fredrick Mwakalebela, Wallace Karia, Emmanuel Kimbe, Shija Richard, Iman Madega na Ally Mayay Tembele, unajua kila mmoja anamtazamo wake na maoni yake kuelekea uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF unaotegemewa kufanyika kesho August 12 katika ukumbi wa mtakatifu Gasper mjini Dodoma.
Mbunge wa Chalinze ambaye pia ni mdau wa soka na shabiki wa club ya Dar es Salaam Young Africans Ridhiwani Kikwete ana maoni gani kuhusu uchaguzi mkuu wa TFF? vipi katika wagombea sita tayari amemuona Rais anayestahili? kama akipewa fursa ya kupiga kura ya kumchagua Rais wa TFF atamchagua nani?.
“Tunawaomba sana wajumbe ambao wanaenda kutuchagulia Rais wa mpira wakachague kiongozi ambaye atasaidia kutimiza ndoto zetu, sisi kama wapenzi wa mpira tuna ndoto nyingi ikiwemo kama kuona mabadiliko makubwa ya kiuendeshaji katika mpira wetu”–Ridhiwani
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0