Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ameendelea na utaratibu wake wa kukagua mradi mmoja baada ya mwingine katika wilaya yake ya Arumeru kuhakikisha unaenda sawa na kwa wakati.
Jerry Muro Jumatano ya October 31 aliungana na wananchi wa Losokito kata ya Mwandeti halmashauri ya Arusha kuhakikisha ujenzi wa shule ya sekondari ya Losiko chini ya nguvu za wananchi unaenda sawa.
DC Jerry Muro alipotembelea ujenzi wa shule hiyo alishika mwiko wa ujenzi ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kujitoa zaidi kuhakikisha lengo lao la kujenga shule ya sekondari kwa jitihada zao linatimia.
Jitihada za ujenzi wa shule hiyo ni kubwa na lengo la wana Arumeru na mkuu wao wa wilaya Jerry Muro ni kuhakikisha ujenzi unakamilika na kuondoa uhaba wa vyumba vya madarasa kwa mwaka 2019 na kuhakikisha shule inaweza kukidhi idadi ya ongezeko la wanafunzi wanaofaulu.
DC Jerry ataendeleana ziara hiyo iliyoanza October 31 na atahakikisha anatembelea kata zote 53 katika ziara hiyo na kutatua changamoto mbalimbali kwa kushirikiana na wananchi wake.