Baada ya Dar es salaam Young Africans kutolewa katika hatua ya mtoano wa michuano ya club Bingwa Africa na Township Rollers ya Botswana, waliangukia katika michuano ya Kombe la CAF na kupangwa kucheza na Wolaitta Dicha ya Ethiopia.
Leo April 7 2018 Yanga waliwakaribisha rasmi Wolaitta Dicha katika uwanja wa Taifa kucheza mchezo wao wa kwanza wa mtoano wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho barani Afrika.
Yanga wakiwa nyumbani watimiza matarajio ya wengi ya kupata ushindi dhidi ya Wolaitta ambao wanaonekana wageni katika michuano hii na ndio mara yao ya kwanza kushiriki hatua hii, kitu ambacho kimeisaidia Yanga kupata ushindi wa magoli 2-0 ambayo yamefungwa na Rafael Daudi dakika ya 1 na Emmanuel Martin dakika ya 54.
Kwa matokeo hayo Yanga watalazimika kwenda Awassa Ethiopia April 18 kucheza mchezo wao wa marudiano dhidi ya Wolaitta wakihitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili wasonge mbele, ila Yanga watalazimika kwenda na tahadhari kwani Dicha hadi wanaingia hatua hii waliushangaza ulimwengu kwa kuitoa Zamalek ya Misri.
Kama Yanga wakifanikiwa kuitoa Waloitta Dicha watarudia rekodi yao ya mwaka 2016 kucheza hatua ya makundi ya michuano hii, baada ya kuitoa Esperanca ya Angola ambapo baada ya hapo ilipangwa kundi moja na TP Mazembe ya Congo, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.
Enzi Samatta alivyokuwa anapiga chenga wachezaji wanne na kufunga VPL