Tanzania Health Promotion Support (THPS) imeadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake huku ikizindua mpango mkakati wake wa miaka mitano (2021-2025).
Shughuli ya kuadhimisha miaka 10 imefanyika Dodoma October 28, 2021 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt Redempta Mbatia ametoa Mhutasari wa mpango mkakati mpya wa THPS 2021 -2025 ambao ni wa pili baada ya ule wa kwanza ulioanza mwaka 2015 na kuisha Desember 2020.
Katika kuadhimisha miaka 10 THPS imeweka vipaumbele vyake ikiwemo utoaji wa huduma za afya, ikijumuisha afua za magonjwa yasiyo ya kuambukiza, VVU, Kifua Kikuu, huduma za VVU kwa Makundi maalumu, utayari katika dharura, afya ya mama na mtoto na maji safi na mazingira.
Kipaumbele kingine ni pamoja na kuboresha huduma za afya, ikijumuisha mifumo ya upatikanaji wa madawa na vifaa tiba, kujengea uwezo watoa huduma za afya na kushirikiana na wizara katika kuandaa sera za afya.
Aidha Ufuatiliaji wa tathmini, ikijumuisha mifumo ya afya, usimamizi wa takwimu, mifumo ya ufuatiliaji na tathmini, mipango ya ufuatiliaji na tathmini, Kipaumbele kingine ni kuongeza uwezo wa Taasisi, ikijumuisha Rasilimali watu, rasilimali fedha, utawala na uongozi, muonekano wa shirika, ubia na wadau wengine, uwajibikaji na uendelevu wa hudumsa.