Afisa mtendaji mkuu Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) mkuu Profesa William Pallangyo amesema taasisi hiyo iko katika mchakato wa kuandika sera ya maswala ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili waweze kutambuliwa na kupewa huduma ya kielimu katika kampasi mbalimbali za taasisi hiyo hapa nchini.
Prof Pallangyo amesema taasisi mbalimbali za Elimu ya juu hapa nchini zimekuwa zina sera zinazosimamia wanafunzi wenye mahitaji maalumu lakini wao kama TIA Wameona bora kuyaboresha ili kuweza kuwafanya wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa maana ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu na walemavu waweze kusoma vizuri.
“kuna mambo kadhaa ambayo inabidi tuyaone kwenye sera yetu kuanzia mwanafunzi anapojiunga chuoni, jinsi tunavyompokea lakini pia jinsi tunavyowafundisha kuna mahitaji ambayo ni muhimu yakaangaliwe, wanahitaji vifaa maalumu, lakini pia wanahitaji majengo ambayo yatawafaa ili waweze kusoma”
Katika hatua nyingine Pallangyo ameongeza kuwa kuna vitu vya ziada ambavyo inabidi taasisi hiyo ivione kama ukiachilia mbali kufundisha na kuna namna ambavyo wanafunzi hao wanapewa mitihani
“Mitihani yao imechapishwa vipi?, je inasomeka kwa wale wenye matatizo ya Uoni hafifu lakini pia na vitu vingine mbalimbali vinavyohusiana na kujifunza kwa ili kuweze kuwa kwa manufaa na waweze kufanya vizuri na hapa nitanbue wanafunzi wenye mahitaji maalumu na wenye ulemavu, wengine wana uwezo mkubwa sana lakini kama hawakuwekewa maandalizi mazuri kwa maana ya mazingira ya kusoma ipasavyo utajikuta hawafanyi vizuri”
katika sera hiyo inayoandaliwa wanafunzi hao maalumu wenye uhitaji maalumu watahakikisha wanawekewa mazingira wezeshi ikiwemo madarasa ambayo yanafikika kiurahisi, uwezo wa kuona ubaoni, vifaa maalumu vya kujifunzia darasani , vifaa vya kuandikia kwa mfano maandishi nundu na vifaa kama hivyo.
“Hayo ni mambo ambayo ambayo kwa pamoja yanatakiwa yaangaliwe kwenye sera yetu ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaojiunga na taasisi zetu za elimu ikiwemo taasisi yetu ya uhasibu Tanzania wanapata fursa ya kuweza kusoma vizuri na waweze baadae kuwa na manufaa kwa taifa letu” alisema Prof Pallangyo.
Pia Lucina Comino mkurugenzi wa huduma za wanafunzi katika taasisi hiyo ya Uhasibu Tanzania amesema ujio wa sera ya kuwatambua watu maalumu wenye uhitaji maalumu utasaidia kwa kiwango kikubwa kuyapata makundi yote wakiwemo walemavu kwenye kampasi za taasisi hiyo.
“Tunaamini Sera hii italeta mageuzi ya kielimu katika vyuo vikuu hivyo wanafunzi wote bila kubagua waweze kupata iliyosawa sambamba na wale watu maalumu wenye uhitaji maalumu kwa wale wenye uwezi na wasio nao hivyo kwa njia yoyote lazima wapate Elimu iliyosawa”
Aidha Comino amesema kabla ya Taasisi ya uhasibu hapa nchini kuwaza na kuja na sera ya watu maalumu wenye uhitaji maalumu hali ilikuwa walemavu na watu maalumu walikuwa wanapewa Elimu na huduma kwa utashi wa yule anaye mhudumia jambo ambalo halitakuwepo baada ya sera hiyo kuanza kufanya kazi