Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka ameshauri mitungi ya gesi kupunguzwa bei ili Watu wengi waweze kumudu kununua na kuongeza idadi ya Watumiaji wa nishati safi ya kupikia.
Akichangia hoja kwenye Kongamano la Kitaifa la Nishati Safi ya Kupikia, Dar es salaam leo, Tibaijuka amesema “Hivi vimitungi vya gesi vimeenea lakini bado havijaenea vya kutosha, kuna Watu wana gesi nyumbani lakini bado wanapikia mkaa, unaweza kuwa na gesi nyumbani ikakuishia ghafla sasa kama hauna jiko mbadala utafanyaje?”
“Hivi vimitungi vya gesi vimeenea lakini bado havijaenea vya kutosha, la pili kuna Watu wana gesi nyumbani lakini bado wanapikia mkaa, wakati mwingine unaweza kuwa na gesi nyumbani ikakuishia ghafla sasa kama hauna jiko mbadala utafanyaje?”- Mama Anna Tibaijuka
“Sasa hivi hiki kimtungi kidogo (cha gesi) bei yake imepanda, naomba nitoe takwimu nikikosea mnikosoe, kilikuwa kinauzwa Elfu 18 kile sasa hivi kinauzwa Elfu 24, Mh. Waziri (Makamba) tatizo linaanzia hapo”- Mama Anna Tibaijuka
“Tatizo linaanzia hapo kwasababu sera za kupeleka jambo hili linataka sera za Serikali, nashukuru Mh. Rais umekuja kuyasikia mwenyewe kwa kujua umuhimu wake, kusudi Watu wachukue kitu lazima uweke utulivu Watu wajipange, Mh. Rais, Mawaziri mtusaide, EWURA na Wahusika waweke bei rafiki ili Kaya ziweze kumudu, Watu wanajua vitu vipo lakini upatikanaji (bei)”- Mama Anna Tibaijuka
“Nimekusikia Mh. Waziri ukisema Taasisi, kuna mahali pa kuanzia, Taasisi, hiyo ipo chini ya uwezo wenu, Taasisi zote zikiambiwa kwamba hakuna kupika na mkaa na kuni zitajipanga lakini zijipange bei iwe nafuu, hapo Serikali ijipange kwa ngazi zote, Halmashauri ziwe na mkakati”- Mama Anna Tibaijuka
“Isije kama directive, ikija kama directive bila support yako Waziri (Makamba) tutashindwa, kwasababu unaweza kutuambia tusipike na kuni lakini kama hatuna mbadala kama hatuna uwezo na hiyo gesi yako tutashindwa, kwahiyo nafikiria ni kitu kizuri lakini unafuu wake na upatikanaji wake utatokana na sera nzuri za kutuongoza”- Mama Anna Tibaijuka