Serikali kupitia kituo cha Uwekezaji Nchini TIC imesema Kwa Mwaka 2023 Imesajili Miradi takribani 504 yenye Mitaji takribani Dola Bilioni 5.6 ambayo ni sawa Tirioni 11 za Uwekezaji hapa Nchini zinazotarajiwa kuleta zaidi ya Ajira 100000 kwa Watanzania.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha uwekezaji hapa Nchini(TIC) ,Bw. Gilead Teri wakati alipofanya ziara ya Kutembelea na kuhamasisha wawekezaji wa ndani ya Mkoa wa Geita ambapo amesema kwa mwaka 2023 walikuwa na wawekezaji wa Mitaji takribani Dola Bilioni 3 na mwaka 2021 walikuwa na Mitaji takribani Dola Bilioni 2.
“Kwa mwaka jana tumesajili Miradi takribani 504 yenye Mitaji takribani Dola Bilioni 5.6 hizi ni zaidi ya tirionin 11 za kiuwekezaji nchini zinazo tarajiwa kuleta zaidi ya Ajira Laki moja kwa watanzania ukilinganisha na mwaka uliopita ambao tulikuwa na uwekezaji wa takribani Dola Bilioni 3 kwa mwaka 2021 takribani Dola Bilioni 2, ” Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC).
Aidha Teri amesema kwa mwaka 2022 walisajili miradi takribani 272 na 73 ambapo kwa mwaka ulioisha wa 2023 wamesajili miradi 504 ni zaidi ya Ongezeko la Asilimia 60 ndani ya Mwaka mmoja huku akisema katika Miradi iliyoongezeka kwa mwaka 2023 takribani nusu ilikuwa ni Miradi ya watanzania ambapo ongezeko hilo limetokana na Mazingira rafiki ya serikali na Wawekezaji.
Nao Baadhi ya Wawekezaji wakubwa ndani ya Mkoa wa Geita akiwemo Mzee Atanas Inyasi Mkurugenzi wa Kampuni ya Blue Coast na Richard Lafael Mkurugenzi wa Gold stone wameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Uwekezaji ambapo imekuwa ni rahisi Mtanzania kuwekeza Maeneo mbalimbali hapa nchini.
Katika hatua nyingine Wawekezaji hao wazawa wamesema kinachofanya watanzania wasiwekeze ni Uoga ambao imekuwa ni changamoto kwa watanzania walio wengi huku wakaiwataka watanzania wenzao kuwa kivutio cha Uwekezaji katika Nyanja mbalimbali.