Ikiwa ni mwendelezo wa Kampeni ya Kitaifa ya Kuhamasisha Uwekezaji wa Ndani imeendesha semina juu ya masuala ya mbalimbali ya Uwekezaji Julai 19, 2024 katika Ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida amepongeza jitihada zilizofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda katika uwekezaji na kuufanya Mkoa wa Mwanza kuwa Mkoa namba mbili nchini kwa uwekezaji.
Amesema hayo alipozungumza na wawekezaji na wafanyabiashara wa mkoa wa Mwanza walioshiriki semina ya kampeni maalum ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani inayoratibiwa na TIC mikoa yote Tanzania ambapo leo wameanza na Jijini la Mwanza.
Kampeni maalum kuhamasisha uwekezaji wa ndani inaratibiwa na TIC mikoa yote Tanzania ambapo leo wako Jijini Mwanza