TikTok ilifanya juhudi za mwisho Jumatatu kuendelea kufanya kazi nchini Marekani, ikiomba Mahakama ya Juu kuzuia kwa muda sheria iliyokusudiwa kulazimisha kampuni mama ya ByteDance yenye makao yake China, kuachana na programu hiyo ya video fupi ifikapo Januari 19 au kukabiliana na marufuku yake.
TikTok na ByteDance ziliwasilisha ombi la dharura kwa majaji kwa amri ya kusitisha marufuku inayokuja ya programu ya mitandao ya kijamii inayotumiwa na Wamarekani wapatao milioni 170 huku wakikata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ulioidhinisha sheria hiyo.
Bunge lilipitisha sheria hiyo mwezi Aprili.
Idara ya haki imesema kuwa kama kampuni ya TikTok inaleta “tishio la usalama wa kitaifa la kina na kiwango kikubwa” kwa sababu ya ufikiaji wake wa idadi kubwa ya data kwa watumiaji wa Marekani,
Kampuni hizo zilisema kuwa kufungwa kwa hata mwezi mmoja kungesababisha TikTok kupoteza takriban theluthi moja ya watumiaji wake wa Marekani na kudhoofisha uwezo wake wa kuvutia watangazaji na kuajiri waundaji wa maudhui na talanta ya wafanyakazi.