Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameilipia timu ya taifa ya nchi hiyo kwenda nchini Brazil kwa ajili ya kuangalia mechi za Kombe la dunia ili kuwahamasisha kufuzu michuano hiyo hapo baadae.
Rais Kenyatta amesema yeye pamoja na mke wake waliahidi kuipeleka timu hiyo baada ya kushinda katika moja ya michuano ya ndani ya nchi hiyo.
Kapteni wa timu Jeremy Onyango amesema hiyo ni ndoto ambayo sasa imetimia kwa timu yake.
Kenya ni moja ya nchi zilizofanikiwa duniani kwa upande wa riadha lakini haijawahi kufika mbali na kufanikiwa kuingia katika michuano ya Kombe la dunia.