Mapema 2017 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohammed Mpinga alitoa agizo kuwa magari yote yaondolewe tinted kwenye vioo vya mbele (front windscreen) huku sehemu zingine tinted inaweza kubakia.
Agizo hilo limekuwa na sura mpya baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo kuagiza magari yote Mkoani humo yaondolewe tinted,hii imeleta mkanganyiko baada ya makamanda wawili kutoa maagizo tofauti.
Ayo TV na millardayo.com ikaamua kukutana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Mohammed Mpinga ambaye anatoa ufafanuzi kuhusu mkanganyiko huo:“Kwa suala la Mkoa wa Arusha kutoa maelekezo ya kutoa tinted kwenye gari lote kwa ujumla ni la Mkoa wa Arusha kulingana na mazingira. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha aliona kuna haja kulingana na matishio ya ujambazi katika Mkoa ule lakini tukizungumzia nchi nzima bado tunafanya tathmini. Kama tukiona kuna haja ya kuendeleza lile ambalo linafanyika Arusha basi tutatoa taarifa kwa wananchi.” – Kamanda Mpinga.
ULIPITWA NA EXCLUSIVE HII??: Kuhusu aliyesali kwa sauti gari lake lisisombwe na maji…amefunga na unaweza kutazama kwa kuplay VIDEO hii!!!