Shirika La Viwango Tanzania TBS limesema kuwa Juice ya Tufaa (Apple) aina Ceres ambayo inazalishwa Nchini Afrika Kusini iliyokuwa inadaiwa kuwa na sumu kuvu bado haijaingia hapa Nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari DSM Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS Lazaro Masasalaga amesema taarifa za uwepo wa juice inayodaiwa kuwa na sumu walizipata kutoka Katika matandao wa Kimataifa wa Mamlaka za Udhibiti Usalama wa chakula taarifa iliyotolewa na mzalishaji mwenyewe.
Kwa mujibu wa Masasalaga mzalisha alitoa taarifa ya kutaka juice hizo ambazo zilizozalishwa June 14 hadi 30 mwaka 2021 zilirudishwe kiwandani ni baada ya kugundua kuwa zina sumu kuvu aina Patulin ambayo husababisha mchafuko wa Tumbo.