Kuna wakati mwingine hata kama una gari lako mwenyewe, ikifika muda wa kurudi nyumbani unajikuta unakosa raha… ishu sio foleni tena, pata picha mvua inanyesha alafu unakuta barabara ya kwenda nyumbani kwako haipo tena !!
Mwezi May 2015 headlines zilizotawala zaidi ilikuwa ishu ya mvua kubwa iliyonyesha mfululizo kwa zaidi ya siku nne Dar es Salaam, leo nimepita barabara ambayo inaelekea maeneo ya Tabata Kimanga… hali sio nzuri maeneo ya Tabata Chama au wengine wanapaita Tabata CCM.
Barabara imekatika kabisa, sasa hivi inaweza kupita gari moja tu tena iwe ndogondogo, kama ikitokea likapita lori la kubeba mizigo basi lolote linaweza kutokea !! Watu nao wameamua kulifanya eneo hilo dampo, kinachofanywa sasahivi ni watu kuendelea kutupa takataka.
Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.