December 10 2017 Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limeelezea kilichosababisha tatizo la ununuzi wa LUKU lililojitokeza juzi na jana nchini.
Demitris Dashina ambae ni Kaimu Meneja Mwandamizi wa Tehama TANESCO amesema tatizo la kununua Luku limesababishwa na wao kutakiwa kuhamisha mifumo kutoka katika jengo la TANESCO Ubungo.
“Mnafahamau tulikuwa kwenye kuhamisha mifumo yetu kutoka jengo linalobomolewa ,sasa imekwenda sehemu ambayo ina usalama wa kutosha na wakati wa kuhamisha kulikua na changamoto ambazo tumezipata ilibidi lazima tuzime mifumo” – Dashina
“Baada ya kuizima ilikuwa lazima ipelekwe inapostahili, kitendo cha kuizima ndio pale ninaposema mtu hawezi kununua LUKU sababu mfumo umezimwa, kabla ya kufikia hali ya uimara leo imetokea hitilafu lakini bahati nzuri timu iko macho, watu wameshaanza kununua umeme mchana wa leo”
Nae Kaimu Meneja Uhusiano Leila Muhaji amesema “Hilo tatizo linaweza kuchukua siku moja au mbili, Wataalamu hawatolala kuhakikisha tatizo linaisha”
HD VIDEO: RAIS MAGUFULI ALIVYOTANGAZA KUWASAMEHE BABU SEYA NA PAPI KOCHA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA