Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepokea taarifa kutoka kwa tume huru aliyoiunda ili kuchunguza malalamiko ya Asma Juma kuhusu kuibiwa mtoto mmoja kati ya mapacha wawili katika hospitali ya Rufaa ya Temeke Dar es salaam.
Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa tume hiyo Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama Dkt. Charles Majige ambapo imeeleza kuwa Asma Juma hakuwa na watoto mapacha kama ilivyodaiwa na mlalamikaji huyo kutokana na kipimo cha Utra sound kukosea katika uchukuaji picha ya mtoto akiwa tumboni.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Charles Majige Amesema kuwa Asma aliamini hivyo kwa sababu Hospitali ya temeke hawakumchukua vipimo vya picha bali walitumia taarifa ya vipimo vya awali .
Aidha Dkt. Majige amesema kuwa tume hiyo imebaini kuwa Asma hakuibiwa mtoto na alikuwa hana mapacha kwa sababu uzito wake ulikua sio wa kubeba watoto wawili na katika chumba cha upasuaji kulikua na wataalamu 6 kutoka vitengo mbalimbali.
VIDEO: Maswali makubwa yaliyosikika Bungeni June 30, 2017, Bonyeza play hapa chini kutazama