Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ametunukiwa heshima ya kuwa “Sir Tony” kuanzia Leo tarehe 1 Januari 2022.
Blair amepewa heshima hiyo katika orodha ya Malkia Elizabeth ya Mwaka Mpya. Katika orodha hiyo watu kadhaa wametunukiwa heshima mbalimbali wakiwemo wataalamu waliopambana na Uviko19.
Aidha Mwanasiasa huyo Mkongwe amewashukuru watu wote walioshirikiana naye katika kazi za kisiasa, kijamii na zingine zote katika kujenga Taifa la Uingereza.