MWANANCHI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick amesema mvua zinazoendelea kunyesha zimevuruga Jiji na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ambapo watu nane wamefariki mpaka sasa.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema Jiji kwa sasa haliko kwenye hali nzuri kutokana na barabara zaidi ya 20 kuaribika, madaraja kadhaa na makaravati kusombwa na maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano kwenye baadhi ya maeneo.
“Nimewaagiza viongozi wa manispaa kufanya kila linalowezekana kurudisha mawasiliano katika maeneo ambayo madaraja yamevunjika ili shughuli ziendelee kama kawaida huku tukijipanga kwa ajili ya kurekebisha maeneo mengine yaliyoathiriwa”— Said Meck Sadick.
Baadhi ya maeneo ambayo yameathirika zaidi kutokana na mvua hizo ni pamoja na Keko, Chang’ombe Maduka Mawili, Yombo Vituka, Vingunguti, Africana, Msasani Bonde la Mpunga, Jangwani, Manzese, Kigogo, Mburahati, Boko na Basihaya.
“Barabara nyingi zimeharibika ingawa Wilaya ya Kinondoni imeonekana kuathirika zaidi, lakini tumeruhusu ziendelee kutumika kupunguza msongamano, ila tutazifunga tena endapo mvua zitaendelea kunyesha ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza, endapo zitatumika zikiwa zimefurika maji”– Meck Sadick.
“Tumefunga kwa muda shule ya Msingi Vingunguti baada ya kuona imezingirwa na maji, hata hao wanafunzi wasingeweza kusoma, lakini maeneo mengine masomo yanaendelea kama kawaida ingawa hali ya maudhurio inaonekana siyo nzuri kutokana na hali ya hewa”—Said Meck Sadick.
JAMBO LEO
Watu wawili wamefariki katika ajali na wengine 11 kujeruhiwa kutokana na ajali iliyotokea maeneo ya Kihonda, Morogoro.
Kamanda wa Polisi Morogoro, Leonard Paul amesema gari hiyo iliyopata ajali ilikuwa ikisafirisha msiba kwenda Kagera kwa ajili ya mazishi, ilipofika eneo hilo iligongana na Basi la Mvula lililokuwa lililotokea Kigoma kwenda Dar.
Kamanda huyo amesema majeruhi wamekimbizwa Hospitali kwa ajili ya matibabu, kwa sasa Jeshi la Polisi linamshikilia dereva wa basi la Mvula kwa ajili ya upelelezi.
HABARI LEO
Hakimu mstaafu wa Mahakama ya Mkoa Arusha, Keenja Manase amepandishwa Mahakama kwa kosa la kughushi nyaraka za Serikali na nyaraka za Serikali na kujipatia Mil. 200.
Manase alisomewa mashitaka hayo matatu mbele ya Mahakimu watatu tofauti, akashindwa kutekeleza msharti ya dhamana kwa Hakimu mmoja, muda mfupi baadae akapandishwa Mahakamani na kusomewa mashitaka mengine.
Shitaka la mwisho kusomewa ilikuwa kesi ya kughushi na kuandika nakala ya barua yenye mhuri wa Jiji la Arusha.
HABARI LEO
Kamati ya Bunge ya PAC imeagiza Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Mafutaa Mohamed kuondolewa Hotelinii ambako amekaa tangu alipoteuliwa ambapo wamedai anaiongezea gharama Serikali.
Kaimu Mwenyekiti wa PAC, Ismail Rage amesema Mkuu huyo wa Wilaya ikifika May 31 itakuwa siku yake ya mwisho kukaa Hotelini hapo, ambapo amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa kuangallia namna ya kumalizia ujenzi wa nyumba ya DC huyo.
Mhasibu wa Mkoa alipohojiwa na Kamati hiyo kuhusu gharama inayotumika kulipia Hoteli hiyo alijibu kwa kigugumizi kwamba wanalipia Tshs. 80,000/- kwa siku kutoka kwenye mfuko mwingine wa Wilaya hiyo.
Mkuu huyo wa Wilaya amekaa kwa miezi miwili Hotelini tangu alipoteuliwa kutokana na nyumba yake kutokamilika kujengwa.
NIPASHE
Jeshi la Polisi Ruvuma linasaka kundi la watu wanaodaiwa kuwa majambazi ambao walivamia na kuwapora pesa na mali zenye thamani ya Mil. 8 watu ambao walikuwa wakielekea msibani Songea vijijini.
Kamanda wa Polisi Ruvuma, Mihayo Miskhela amesema siku ya tukio Mei 7 kundi hilo la watu wakiwa na marungu na mapanga waliweka magogo na mawe barabani na kuliteka basi lililokuwa likisafirisha msiba huo na kuwapora vitu hivyo watu 22 waliokuwa wakisafirisha msiba.
Kamanda huyo amesema kuwa kundi hilo la watu tisa waliteka pia gari nyingine ikiwemo lori na gari ndogo pia na kuwapora vitu mbalimbali.
Watu hao waliwakamata na kuwapekua watu wote waliokuwa kwenye magari hayo huku wakiwa wamejifunga vitambaa vyeusi usoni na kisha kutokomea kusikojulikana.
NIPASHE
Kamati ilizoundwa kuchunguza tuhuma dhidi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi imebaini kuwa hakuwa na makosa yoyote ya Kimaadili yaliyohusu sakata la ESCROW ambapo Katibu Mkuu huyo alisimamishwa kazi Desemba 23 2015 ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.
Katika sakata hilo wengine waliosimamisha ni aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, pamoja na Wabunge Andrew Chenge na William Ngeleja.
“Mchakato wa kinidhamu, kimaadili na kijinai dhiidi yake umefikia mwisho.. Mwenye Mamlaka ya Uteuzi atatafakari taarifa hizi na kuamua cha kufanya kuhusu ajira yake..”— aliongea Balozi Ombeni Sefue wakati akisoma ripoti hiyo.
Taarifa nyingine ya Tume iliyoundwa kuchunguza sakata la Oparesheni Tokomeza imeonesha viongozi ambao walisimamishwa kupisha uchunguzi wa sakata hilo hawakuhusika moja kwa moja, na kama nafasi zao zingekuwa wazi wangerudishwa.
Viongozi hao yuko aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, David Mathayo na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
Wakati akitoa ripoti hiyo, Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa wakati wa utekelezaji wa Oparesheni hiyo Desemba 2013 kulipatikana mafanikio makubwa hivyo tuhuma na malalamiko yaliyotolewa hayakuwa ya msingi.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.