Mshambuliaji mpya wa Atletico Madrid, Fernando Torres anaweza kuwa bado hajaanza kuitumikia klabu yake lakini tayari ameshaanza kuvunja rekodi tofauti tangu usajili wake kutoka AC Milan ulipokamilika.
Utambulisho wake mbele ya mashabiki ndani ya uwanja wa Vicente Calderon ulikusanya mashabiki 45,000 idadi ambayo haijawahi kuonekana katika utambulisho wa mchezaji raia wa Hispania.
Jezi namba 19 ambayo Fernando Torres amekabidhiwa hadi sasa inafanya vizuri sana sokoni ambapo mashabiki wa Atletico Madrid wamekuwa wakiinunua kama njugu ambapo ndani ya siku ya jumapili pekee duka rasmi la klabu hiyo jijini Madrid liliuza jezi 200o ambayo ilikuwa rekodi nyingine ikiwekwa na mshambuliaji huyo.
Fernando Torres aliwahi kuwa mchezaji wa Atletico miaka kadhaa iliyopita na mashabiki hawajaridhika kuvaa jezi yake ya zamani bali wamesisitiza kununua jezi yake mpya ambayo atakuwa anaivaa katika kipindi hiki.
Torres anatarajiwa kuanza kuitumikia Atletico Madrid kwenye mchezo dhidi ya Real Madrid utakaopigwa hapo kesho katika michuano ya Copa Del Rey.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook