Mnamo Juni 13, alipaswa kuhukumiwa, kifungo chake rasmi gerezani, kuhusu kukutwa na hatia katika kesi yake ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion na zaidi ya hayo, waendesha mashtaka waliomba angalau miaka 13 kutumika, kwa rapper huyo lakinihukumu ya Tory iliendelea kuahirishwa kwa mara nyingine, hadi Agosti 7.
Wakati huo huo, Tory anatoa feedbackk kwa mashabiki zake kutoka gerezani, kwa mara nyingine tena na alitumia ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumapili, kuelezea jinsi ameweza kufanya jela yake kuwa aina ya ofisi, na pia kurekebisha akili, mwili na roho yake, akiwa kizuizini kwa muda wa miezi saba iliyopita.
Zaidi ya hayo, Tory alifichua kuwa ngoma yake mpya ataiachia Jumatatu, saa sita usiku inayokwenda kwa jina “Hurts Me”, akimshirikisha Yoko Gold.