Shirika la habari la BBC limeripoti kuwa, Mwanamke mmoja aliyemtelekeza mwanawe ndani ya karatasi ya plastiki katika bustani moja nchini Uingereza amenusurika na adhabu ya kifungo jela.
Mtoto huyo mchanga aliyekuwa wa siku moja tu, alikutwa na mtu aliyekuwa anamtembeza Mbwa wake katika bustani hilo.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27, alihukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita na kuwekwa chini ya ulinzi wa maafisa wa kijamii kwa miaka miwili.
Hata hivyo alikiri kumtelekeza mtoto wake kwa makusudi na kusema kuwa aliathirika kimawazo baada ya kujifungua mtoto huyo mwezi Mei.
Polisi walisema kuwa mtoto huyo alinusurika kifo kwa dakika thelathini tangu kutelekezwa kwani alipatikana haraka sana na kwamba mwili wake tayari ulikuwa umeanza kuwa baridi.
Mtoto huyo alipatikana mwaka jana akiwa amefungwa ndani ya taulo na kuwekwa ndani ya karatasi ya Plastiki katika bustani hilo.
Mama huyo aliambia mahakama kuwa alifanya kitendo chake katika hali ya kutojielewa.
Pia alifahamisha mahakama kuwa alijifungulia mtoto wake katika sakafu ya bafu nyumbani kwa mamake hali ambayo ilimuathiri kimawazo.
Alificha ujauzito wake kutoka kwa familia yake na pia hakuwahusisha madaktari kwa sababu alihofia kuwa hangeweza kustahamili ujauzito wake.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB