Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu amesitisha kwa muda ukusanyaji wa ada za maegesho ya magari kwa kutumia mfumo mpya wa kieleketroniki.
Mfumo huo unasimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura).
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Nteghenjwa Hosseah imeeleza kuwa Waziri Ummy amesitisha mfumo huo kuanzia leo Jumamosi Oktoba 9, 2021 na kuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Professa Riziki Shemdoe kukutana na timu ya wataalamu Tarura kujadili namna ya kutatua changamoto changamoto zilizojitokeza.
Soma zaidi: Ada maegesho ya magari Dar kulipwa kwa mtandao
“Wakati hayo yakiendelea ukusanyaji wa ada za maegesho ya magari zitaendelea kukusanywa kwa kutumia mfumo wa awali (Manual system) ambao ulikua unatumika kukusanyia ada hiyo kabla ya kuanza kutumia mfumo wa kielektroniki (TeRMIS)” imeeleza taarifa hiyo.