Mkurugenzi wa Masoko kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Dk. George Fasha anasema wanaboresha ushoroba wa kati unahudumia nchi za Burundi, DRC, Rwanda na Uganda Ili kuongeza ufanisi zaidi kwenye sekta hiyo
Dk. Fasha amesema ukuaji wa biashara uliopo kwa sasa ni mkubwa ambao unailazimu TPA kuona namna ya kuboresha masuala ya ushoroba wa kati na kukabili changamoto zilizopo ili kufikia soko kubwa lililopo kwenye ushoroba wa kati.
Amesema bandari ya Dar es salaam imekuwa ikihudumia tani mil 25, Mtwara zaidi ya tani Mil 3 na Tanga imekuwa ikivutia mzigo kwa kiasi kikubwa baada ya kujengwa gati ya mita zaidi ya 450 na kupokea meli kubwa kwa sasa sambamba na kuongeza kina kutoka mita 3 hadi 13 na kutanua njia ya kuingilia meli.
Kwa upande wake mwenyekiti wamiliki wa Malori Tanzania (TAMSTOA) Chuki Shabani ameomba jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani nchini kuona haja ya kuacha kuchelewesha magari ya mizigo kwa kuyazuia yanapokuwa na makosa madogo yanayolipika hata baada ya kurudi ili kulinda usalama wa soko la mizigo nchini.
Mwenyekiti huyo amesema hayo kwenye mkutano wa wadau wa ushoroba wa kati uliofanyika mkoani Morogoro ambapo alisema serikali itakusanya mapato lakini mzigo ukicheleweshwa njiani na usipofika kwa wakati unapokwenda mteja wa bandari anaweza akabadilisha bandari na kutumia nyingine na serikali kukosa zaidi hayo mapato