Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imedhamiria kufanikisha maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kufanya mageuzi makubwa ya Uchumi wa nchi kutoka daraja la tatu kwenda kwenye nchi zenye uchumi wa daraja la pili.
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 13, 2022 na Mkurugenzi Mkuu Plasduce Mbossa katika kikao kazi na wahariri kilichofanyika kwenye hoteli ya Stella Maris Bagamoyo Mkoa wa Pwani na kuhudhuriwa na watendaji mbalimbali wa TPA.
“Uwepo wa bandari zenye uwezo mdogo na ufanisi wa chini ni kikwazo kikubwa kwa shughuli za uzalishaji na biashara ambacho kinaongeza gharama za huduma za bandari ambazo zinaishia kulipwa na walaji ambao ni Wananchi wa kawaida wakati wa kununua huduma na mahitaji yao ya kila siku”- Mkurugenzi Mkuu Plasduce Mbossa