Leo March 16, 2018 Serikali ya Tanzania imenunua rasmi vichwa vya treni 11 vikiwa na thamani ya USD Milioni 2,400,000 kutoka kampuni ya Progress Rail Locomotive (PRL).
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa manunuzi hayo, Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema ununuzi wa vichwa hivyo utaongeza ufanisi.
Amesema mnamo mwaka 2015 serikali ilinunua vichwa kama hivyo 13 namba 9001 hadi 9013 kwa bei ya USD Milioni 3,200,000 kwa kichwa kimoja.
“Kamati ilifanya majadiliano ya bei na kufikia muafaka wa kununua vichwa 11 kwa USD Milioni 2,400,000 kwa kichwa kimoja ambayo ni pungufu ya Dola 800,000 kwa kila kichwa cha treni kuli”-Kadogosa