Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 4.9 na 4.3 katika kipimo cha richter limetokea kwenye Mikoa ya Singida na Dodoma leo February 17, 2023.
Akithibitisha taarifa hizo Mjiolojia Mwandamizi kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Gabriel Mbogoni amesema kuanzia jana yametokea matetemeko ya ardhi matatu, moja lilitokea maeneo ya mpaka wa Singida na Dodoma likiwa na ukubwa wa 4.9 katika kipimo cha richter, jingine lilitokea asubuhi ya leo likiwa na ukubwa wa 4.3 likifuatiwa na lenye ukubwa wa 4.9 na haya mawili yametokea katika Wilaya ya Manyoni.
Hata hivyo Mbogoni amesema mpaka sasa hakuna taarifa zozote za madhara ambayo yamesababishwa na matetemeko ya ardhi ambayo yametokea toka jana.