Leo May 3 2017 makao makuu ya timu ya Simba SC Kariakoo Dar es Salaam, Rais wa timu hiyo Evans Aveva ameongea na waandishi wa habari kuhusu kamati ya haki na hadhi za wachezaji kuipokonya Simba point 3 ilizokuwa imepewa na bodi ya Ligi kutoka kwa Kagera Sugar kwa kumchezesha mchezaji Mohamed Fakhi aliyekuwa anadaiwa kuwa na kadi 3 za njano.
Kuhusiana na maamuzi hayoa yaliyotolewa na TFF kupitia kwa katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa na kusema Simba haiwezi kukata rufaa tena, Rais wa Simba Evans Aveva ametangaza msimamo wao ikiwemo kwenda FIFA na kulipeleka suala hilo katika mahakama ya kimichezo CAS.
GOAL & HIGHLIGHTS: Simba vs AzamFC April 29 2017, Full Time 1-0