Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Iringa Imeendelea Kuwatembelea na kuwashukuru walipakodi mbalimbali Mkoani hapa kwa kuendelea kutimiza wajibu wao wa kulipa Kodi kwa wakati
Shukrani hizo zimetolewa leo 17.12.2024 baada ya Meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania Mkoa wa Iringa Bw. Peter Jackson akiwa ameambatana na meneja msaidizi Bw. Gwamaka Pholld walipomtembelea mlipakodi ASAS GROUP OF COMPANIES.
Meneja amesema “Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa. Na wafanyabiashara hasa kwenye ukusanyaji wa mapato,na Naomba nifikishe kwako Salam za Kamishna Mkuu ambaye amesema yupo bega kwa bega na walipakodi wote na awatakia Heri ya sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya”
Naye Mkurugenzi Mtendaji Wa Kampuni hiyo Bw.SALIM F. ABRI ameishukuru TRA kwa ushirikiano inaotoa wa wadau wake na ameongeza kusema kwamba
“Asas imeanza kulipa kodi tangu mwaka 1951 hivyo tunatambua umuhimu wa kulipakodi ya serikali, na tunaomba kila mfanyabiashara alipe kutokana na faida itokanayo na biashara yake” pia Bw SALIM ameshauri serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania iweke jitihada za makusudi kabisa kuhakikisha inakusanya kodi ya ushuru wa bidhaa kutoka kwa waagizaji/waingizaji wa bidhaa kupitia mipaka yote ya nchi yetu.