Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Iringa imeendelea kuwatembelea na kuwashukuru walipakodi mkoani hapa kwa kuendelea kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati na kwa hiyari sambamba na shukrani hizo Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa amewataka Wafanya biashara kuzingatia sheria zote za kodi, na amewataka wafike ofisini wanapokuwa wa changamoto yoyote ya kukodi kwa utatuzi wa haraka.
Hayo yamesemwa leo na Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa BW. Peter Jackson akiwa ameambatana na Meneja Msaidizi wa Ukaguzi na ufuatiliaji ambapo walimtembelea mfanyabiashara na mzalishaji wa Bidhaa mbalimbali wa IVORY , IRINGA FOOD AND BEVERAGES LIMITED Bw . Suhail Thakore Kwaajili ya kumshukuru kwa ulipaji wa kodi kwa hiyari
Hata hivyo Bw . Suhail Thakore ameishukuru TRA kwa ushikiano mzuri na wafanyabiashara na ameomba ukaribu huo uimarishwe zaidi pia ameiomba Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania iongeze usimamizi wa matumizi wa Mashine za EFD ili kila mfanyabiashara achangie kodi stahiki.