Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa Morogoro imewataka wafanyabishara wenye malimbikizo ya madeni kufika katika ofsni hizo kwaajili ya kuingia makubaliano ya namna kulipa madeni yao.
Akizungumza na waandishi wa habari meneja wa TRA mkoa Morogoro Syver Rutagwelera amesema wafanyabishara wenye Changamoto hiyo wanatakiwa kuwasiliana na mamlaka ili changamoto zao ziweze kutatuliwa badala ya kufunga biashara zao na kukimbia.
Rutagwelera amesema TRA Morogoro inaendelea kuadhimisha wiki ya shukrani kwa mlipakodi ambayo imeanza Novemba 27 hadi Desemba Mosi mwaka huku, kitaifa yakiwa yamefanyika Novemba 24 mwaka huu lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa wafanyabishara kuwafikia moja kwa moja pamoja na kutoa elimu kwa jamii kutambua umuhimu wa kulipa kodi.
Katika kuadhimisha siku hiyo TRA Morogoro imetoa msaaada wa vitu mbalimbali kwa wenye uhitaji ikiwemo kituo cha watoto wenye changamoto ya akili na viungo Mehayo kilichopo Mazimbu na gereza la Mifugo Mtego wa Simba .
Akikabidhi msaada huo Meneja Msaidizi Huduma kwa Mlipa.Kodi Chacha Gotora amesema wameamua kurudisha kwa jamii lengo kuhamasha wananchi kuona umuhimu wa kulipa kodi Kwa hiari kwa ajili ya ujenzi wa Taifa ambapo vitu vyote vina thamani zaidi ya Shilingi milioni tatu
Akizungumza kwa niaba ya gereza mkuu wa gereza hilo SSP. Nicostratus Magoro ameshukuru TRA Morogoro na kutoa wito Kwa wadau wengine kuiga mfano huo kwani kuna baadhi ya watu wanaorekebishwa tabia katika gereza hilo hawatembelewi kabisa na ndugu zao hivyo kukosa mahitaji muhimu huku Miriam Bosco kwaniaba ya kituo cha Mehayo akishukuru TRA huku alibainisha changamoto inayowakabili kuwa ni upungufu wa chakula ukilinganisha na idadi ya watoto waliopo ambao ni 45 .