Kama ulipitwa na hii stori iliripotiwa kwenye habari ya kituo cha ITV leo kuhusu ishu ya kufikishwa Mahakamani kwa watuhumiwa kutoka Mamlaka ya TRA ambao walisimamishwa kazi kutokana na kuhusishwa na tuhuma za upotevu wa makontena 349 bandarini Dar.
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alipita bandarini siku ya Ijumaa November 27 2015 na kukutana na hiyo ishu ya makontena hayo kupotea na pia kubaini kuwepo kwa ubadhirifu ambao umepelekea Serikali ya Tanzania kukosa mapato kupitia kodi… Jeshi la Polisi likapewa jukumu la kuwakamata watumishi hao 12 na kuendelea na taratibu nyingine za kuwawajibisha.
Leo watuhumiwa nane kati wa kesi hiyo wamefikishwa Mahakama ya Kisutu na kusomewa mashtaka ya kesi zao, baadae kesi ikaahirishwa mpaka December 17 2015 ambapo Mahakama hiyo ilikataa kuwapa dhamana watuhumiwa wote.
#MillardAyoUPDATES: Watuhumiwa kesi ya upotevu makontena 349 bandarini Dar wasomewa mashtaka mahakama ya Kisutu, Mahakama yawagomea dhamana.
— millard ayo (@millardayo) December 4, 2015
Hapa ninazo picha kutoka Blog ya Issa Michuzi ilivyokuwa Mahakama ya Kisutu leo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFB YOUTUBE