Baada ya bunge la bajeti kumalizika hivi karibuni ambapo Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 inapanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 29.54 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo.
Shughuli ya makusanyo ya mwaka mpya wa fedha imeanza ambapo leo August 5 2016 Mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA’ imetoa taarifa kwamba imekusanya kiasi cha trilioni 1.055 sawa na asilimia 95 kwa kipindi cha July 2016. Katika mwaka huu wa fedha TRA imepewa lengo la kukusanya shillingi trilioni 15.1 ikilinganishwa na lengo la trilioni 13.32 kwa mwaka ulioisha.
Akizungumza na waandishi wa habari, mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi, Richard Kayombo amesema TRA imeboresha zaidi mifumo yake ili kupunguza kabisa changamoto za kutopatikana kwa mtandao ambayo mara nyingi huathiri makusanyo sasa wameunganisha mifumo ya TRA na mamlaka ya bandari Tanzania ilikuhakikisha mapato yote ya serikali yanakusanywa kwa wakati na usahihi.
TRA imezidi kukumbushia kudai risiti unaponunua bidhaa na kutoa risiti unapuuza bidhaa ambapo wamesema kwamba kutotoa risiti na kutodai risiti ni makosa kwa mujibu wa sheria na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kutotoa risiti na kudai risiti.
ULIKOSA HII YA KIWANDA KUPIGWA FAINI YA MILIONI 30 KISA MAJI TAKA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI