Albamu ya “Utopia” iliyosubiriwa kwa muda mrefu ya Travis Scott inaonekana kuwasili hivi karibuni huku tukio la uzinduzi wa albamu ya Utopia likitarajiwa kufanyika Cairo, Misri, kwenye Pyramids of Giza.
Utopia itakuwa na kazi 5 binafsi za sanaa, vinyls, CD na maagizo ya mapema[set pre-orders].
Zaidi ya hayo, Travis pia ataperform albamu yake pia.
Travis amekuwa akifanya kazi kwenye album yake ya Utopia tangu 2020, lakini tarehe rasmi ya kutolewa iliendelea kusogezwa mbele.
Utopia itakuwa albamu ya kwanza ya Travis Scott katika karibu miaka mitano.
Album yake nyingine ilitoka mnamo Agosti 2018, ambayo ilikuwa “Astroworld.”
Project hiyoilikuwa na wimbo bora zaidi wa Billboard Hot 100 na certified diamond single ulioidhinishwa kuwa “Sicko Mode” akimshirikisha Drake.
Mwishoni mwa 2021, Travis aliendelea kuachia nyimbo kadhaa ambazo zinaweza kuwa kwenye Utopia, ambazo ni “Mafia” na “Escape Plan.”