Wiki hii kumekuwa na taarifa ambayo iliandikwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa askari wa usalama barabarani anatakiwa kukamata makosa yasiyopungua kumi kwa siku, leo June 08 2016 kamanda wa usalama barabarani Mohamed Mpinga amelitolea ufafanuzi jambo hilo………
>>>jeshi la polisi halijawahi kuwaelekeza askari wake kukamata kiwango cha makosa kumi kila siku barabarani askari wameelekezwa wakamate makosa mengi iwezekanavyo kutokana na kuendelea kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba madereva wengi barabarani hawazingatii sheria za usalama barabarani na hivyo kusababisha ajali barabarani.
>>>Jeshi la polisi haliwezi kuweka kiwango cha idadi ya kukamata makosa wakati madereva wanaendelea kufanya makosa barabarani na ajali zinaendelea kutokea, ieleweke kwamba makosa ya usalama barabarani ni uhalifu unaofanywa na madereva wanapotumia barabara ambao ni sawa na uhalifu mwingine.
KAMA UKIKAMATWA NA TRAFIKI KWA KUPITA NJIA YA BRT UTAKUMBANA NA ADHABU, BONYEZA PLAY HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE