June 8 2016 Serikali kupitia Wizara ya fedha na mipango imewasilisha bungeni Dodoma mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2016. Jukumu la kuwasilisha limefanywa na Waziri Philip Mpango.
Baada ya kumalizika kwa uwasilishaji huo, Naibu spika Tulia Ackson akasimama kusoma mwongozo kuhusu wabunge wanaotoka nje ya bunge huku wakiendelea kupokea posho.
‘Mbunge anatakiwa kulipwa mshahara au posho kulingana na kushiriki mijadala ya bunge, kususia au kutotimiza wajibu wake na si halali kupokea malipo‘
‘Natamka kuwa wabunge waliotoka nje ya ukumbi kwa shughuri zisizokuwa rasmi hawastahili kulipwa posho kwa siku zote ambazo watakuwa nje mpaka tutakapotangaza utaratibu mwingine ‘
ULIIKOSA HII? SERIKALI IMETANGAZA KUTENGA TRILION 29.5 KAMA BAJETI YAKE KUU KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE