Hatimae serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya uchukuzi imesaini mkataba wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa Reli ya kisasa itakayowezesha Treni zinazotumia umeme kuanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza Tanzania.
Waziri wa uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema ‘Sasa hivi kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza unatumia saa 36 ambapo kuna kilometa 1219 lakini Treni mpya za umeme zikianza kufanya kazi safari itakua rahisi zaidi‘
‘Leo tunashuhudia utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa sehemu ya kipande cha reli kati ya Dar es salaam na Morogoro chenye urefu wa kilometa 300 na mkataba huu utakua baina ya RAHACO kampuni hodhi ya rasilimali za reli na ubia kati ya kampuni ya UTURUKI na URENO’
‘Itakua kwa gharama ya USD BILIONI 1, Milioni 215, laki 2 na 82 ikijumuisha VAT USD Milioni 185 na laki 3, hii ni kwa ajili ya gharama za ujenzi kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro‘
‘Katika Afrika Treni kubwa ambayo itakwenda spidi kubwa itakua ni ya Tanzania (Kilomita 160 kwa saa), Treni nyingine itayokua na spidi kubwa itakua ni Morocco itakua kilometa 200 kwa saa, naamini na sisi Tanzania tutabadilisha mawazo kwenye Treni ya Dar Mwanza tutakua Kilometa 200 kwa saa‘
Kama hufahamu, wakati wa utawala wa Uingereza marekebisho kidogo yalifanyika kwenye usafiri wa Treni Tanzania kutoka Treni inayotumia mvuke kuja kwenye injini ya Diesel, hata hivyo miundombinu hii kwa sasa ni chakavu na mwendokasi sio chini ya Kilomita 30 kwa saa ambayo kutoka Dar kwenda Mwanza unachukua saa 36‘ – Profesa Mbarawa
‘Mda wa mradi huu wa Umeme kukamilika ni miaka miwili na nusu baada ya ujenzi kuanza, kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro Treni mpya ya umeme itatumia saa moja na dakika 16, Dar es salaam kwenda Dodoma itakua masaa mawili na nusu, Dar-Mwanza saa saba na nusu’ – Profesa Mbarawa
ULIPITWA? Tazama ajali ya Treni iliyotokea Tanzania, Mabehewa yakiondolewa na Reli ikirekebishwa Ruvu Pwani, play kwenye hii video hapa chini