Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameahidi kukomesha kile alichokiita “upuzi wa watu wanaobadili jinsi zao” siku ya kwanza tu atakapoingia madarakani.
Kauli hiyo ameitoa wakati Warepublican wanaotarajiwa kudhibiti mabunge yote mawili ya Marekani-wakiendelea na juhudi zao za kupinga haki za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja LGBTQ.
Trump amesema atasaini agizo la kiutendaji kukomesha ukeketaji wa watoto na kuwaondoa watu waliobadili jinsia zao jeshini na mashuleni.
Kiongozi huyo ameahidi pia “kuwazuia wanaume kushiriki michezo ya wanawake” na kuongeza kwamba itakuwa sera rasmi ya Marekani kuwepo kwa jinsia mbili pekee, mwanamume na mwanamke.
Suala la watu waliobadili jinsia zao limezua mjadala mkubwa wa kisiasa huku Warepublican na Wademocrats wakionyesha msimamo tofauti juu ya sera kama vile matibabu na aina ya vitabu vinavyoruhusiwa kwenye maktaba za umma au shule kuhusu maudhui ya mapenzi ya jinsia moja.