Rais wa zamani Donald Trump, mwenye umri wa miaka 77, tayari ametangazwa mshindi wa majimbo tisa na vyombo vya habari kadhaa vya Marekani: Virginia, North Carolina, Oklahoma, Tennessee, Alabama, Arkansas, Texas, Maine na Massachusetts, Minnesota na Colorado.
Donald Trump ameshinda majimbo kumi na moja ya kwanza hatarini siku ya Jumanne katika siku kuu ya uchaguzi ya Super Tuesday, na kuthibitisha ukali wake wa ushindi kuelekea uteuzi wa chama cha Republican dhidi ya mpinzani wake Nikki Haley.
“Asante – MAGA!” “, ameandika Donald Trump kwenye jukwaa lake la Truth Social, akitumia kifupi cha kauli mbiu yake “Make America Great Again” na kuorodhesha majimbo ambayo alishinda. Tangu Januari 15 na licha ya matatizo yake yanayomkabili mahakamani, ameshinda karibu kura zote za mchujo zilizoandaliwa na chama chake. Chama cha Democratic kinasema kimepokea vema ushindi huo na kimetoa wito kwa kami yake kwa michango na kuwa makini zaidi.
“Super Tuesday” ni tukio muhimu katika siasa za Marekani, ambapo majimbo 15 hupanga kura za mchujo wao wa urais kwa wakati mmoja. Mamilioni ya Wamarekani walipiga kura kuwateua wagombea wao wa Democratic na Republican katika uchaguzi wa mwezi Novemba.
Matokeo ya Super Tuesday hii yanatarajiwa usiku kucha, huku vituo vya mwisho vya kupigia kura vikitarajia kufungwa saa 11 alfajiri saa za kimataifa huko Alaska.