Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alifika siku ya Alhamisi (Agosti 24) katika gereza moja huko Atlanta, katika jimbo la Georgia nchini Marekani na aliwekwa chini ya ulinzi kwa muda mfupi kama sehemu ya mashtaka yake juu ya ushawishi wake wa uchaguzi mwaka 2020 katika jimbo hili.
Donald Trump alijitokeza katika jela moja huko Atlanta, Georgia, Alhamisi kufuatia kushtakiwa kwake mapema mwezi huu kama sehemu ya uchunguzi wa juhudi zake za kupotosha matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 katika jimbo hili muhimu. Alishindwa kwa kura ndogo na rais wa sasa kutoka chama cha Democratic Joe Biden.
Trump, ambaye aliachiliwa kwa dhamana, na kuondoka muda mfupi baadaye, alishtakiwa mapema mwezi huu kwa kukiuka sheria za jimbo la Georgia za ubadhirifu na “kutenda uhalifu mwingine, akikbiliwa na mashtaka 13 katika jimbo la Georgia.”
Alhamisi, alichukuliwa alama za vidole na picha yake akiwa jela, maarufu kama Mug Shot, ikapigwa, wasaidizi walisema.
Alitumia takriban dakika 20 ndani ya jela ya Kaunti ya Fulton, ambapo sherifu aliahidi kumshughulikia kama mfungwa wa kawaida: Rais wa 45 wa Marekani pia alipata nambari yake ya gereza PO1135809 na alama zake za vidole zilizosajiliwa, anaripoti mwandishi wetu maalum huko Atlanta, David Thomson.
Hili ni tukio la kihistoria kwa mara ya kwanza kabisa kwa rais wa zamani wa Marekani, kutoka chama cha Republican kuwekwa chini ya ulinzi kwa muda mfupi, akipimwa uzito, na kupigwa picha kabla ya kuachiliwa kwa dhamana. Hii ni picha ya kwanza ya rekodi za polisi ya rais wa zamani wa Marekani