Rais wa Marekani Donald Trump ametumia ukurasa wake wa Twitter kulalamika kuwa, anaongoza kwa kura nyingi lakini wanachofanya ni kumuibia ili asishinde .
“Tunaongoza kwa kura nyingi, lakini wanajaribu kutuibia, hatuwezi kuwaruhusu wafanye hivi, kura haziwezi kuhesabiwa baada ya vituo kufungwa ” Trump
Huenda Wamarekani wakakesha Jumatano kabla ya kujua nani atakuwa rais wao mpya kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo kwenye uchaguzi huu uliofanyika wakati taifa hili limegawika sana kwa mara ya kwanza tangu vita vya Vietnam miaka 1970.
Kura zinahesabiwa katika majimbo yote hivi sasa na katika majimbo ya mashariki inaonekana wagombea hao wawili wanapata ushindi katika ngome zao za kawaida wakati ushindani uko katika majimbo mengi na imekuwa vigumu kutabiri nani atapata ushindi.
Marekani ushindi unategermea zaidi katika majimbo kwani kila mmoja anagombania wajumbe wa majimbo hayo kuweza kushinda uchaguzi. Kuweza kupata ushindi mgombea kiti cha rais anahitaji kupata kura 270 za wajumbe wa majimbo.
UWEZO WA KOMANDO WA JWTZ, UTABAKI MDOMO WAZI