Rais wa Marekani Donald Trump ameusaini muswada wa sheria wa dola bilioni 900, unaokusudia kutoa misaada kwa watu walioathiriwa na janga la virusi vya corona
Kwa siku kadhaa rais Trump alikataa kutia saini muswada huo tangu ulipopitishwa wiki iliyopita na bunge akiutaja kuwa fedheha.
Kulikuwa na wasiwasi kwamba kuchelewa kufanya hivyo, kungesababisha baadhi ya faida za ukosefu wa ajira kupotea, ikimaanisha kwamba mamilioni ya watu wangeweza kupoteza pesa wakati huu mgumu wa uchumi uliochangiwa na janga la virusi vya corona.
Mpango huo unaotoa misaada ya dharura ya janga la virusi vya corona, ni sehemu ya muswada mkubwa wa matumizi ambao pamoja na saini ya Trump, utasaidia kuepusha shughuli za serikali kufungwa.
“Ninasaini muswada huu kurejesha manufaa ya ukosefu wa ajira, kuzuia watu kuondolewa kwenye nyumba, kutoa misaada, kuongeza pesa katika programu za ulinzi wa malipo, kurudisha wafanyakazi wetu wa ndege kazini, kuongeza pesa zaidi katika usambazaji wa chanjo na mengi zaidi” Trump katika taarifa yake wakati wa mapumziko ya Krismasi huko Florida.
HOTEL YA SUGU KUBOMOLEWA, RAIS MAGUFULI AZUIA “MSIBOMOE HOTEL SUGU, MSILETE SIASA”