Rais Donald Trump wa Marekani amesema Marekani inazo mashine nyingi za kusaidia wagonjwa kupumua (ventilators) tena za kisasa na zenye ubora wa hali ya juu, na kusema kwa sasa wana uwezo wa kusaidia Nchi nyingine zenye uhitaji, hivyo amefungua njia kwa Nchi zenye uhitaji kuwasiliana na Nchi hiyo na atawapatia.
“Tunazo Ventilators za kutosha, nimeongea na Waziri Mkuu Ethiopia Barani Afrika, Nchi yao inataka ventilators, tutawapa”-Rais Trump wa Marekani
Trump pia amesisitiza kuwa ni umuhimu kwa Nchi mbambali kuongeza juhudi katika kuwapima Watu wake virus vya corona huku akitolea mfano wa Marekani ambayo amesema imewapima Watu wengi hadi kufikia hivi sasa.
“Ni kujidanganya kwa kuamua kusema una idadi ndogo ya visa vya corona wakati kiwango cha upimaji kipo chini, Marekani sasa tumewapima zaidi ya Watu Million 5, hii ni zaidi ya Nchi yoyote Duniani na hata Mataifa makubwa yakiungana idadi ya Watu waliowapima haitufikii”-Rais Trump wa Marekani