Rais mteule wa Marekani Donald Trump huenda akapitisha amri ya utendaji ambayo itawafukuza wanajeshi waliobadili jinsia kutoka jeshini na anaripotiwa kujiandaa kutia saini agizo kuu ambalo litawazuia watu hao kupata huduma za kiafya katika jeshi, mapema siku yake ya kwanza atakaporejea ofisini kufuatia kuapishwa kwake mnamo Januari 20.
Trump, katika muhula wake wa kwanza, alisema kwamba Marekani”haitakubali tena au kuruhusu” watu waliobadilisha jinsia katika jeshi, huku akitoa “gharama kubwa za matibabu na usumbufu unaopatikana kwaajili yao ambapo Marufuku hiyo ilianza kutekelezwa mnamo 2019 Walakini, Rais Joe Biden alibadilisha sera hiyo baada ya kuchukua wadhifa huo.
Haya pia yanajiri wakati Trump akiendelea kukosoa kile anachokiita sera za “uamsho” katika jeshi huku hatua hiyo ikitajwa kuwa huenda itawaondoa kimatibabu wanachama 15,000 wa huduma ya jinsia kutoka kwenye jeshi na kuwatangaza kuwa hawafai kuhudumu jeshini.
Maagizo hayo pia yataweka marufuku kwa wanachama waliobadili jinsia kujiunga na jeshi, na hii inakuja wakati karibu matawi yote ya jeshi la Marekani yanajitahidi kufikia malengo ya kuajiri hivi karibuni.
Trump, mwenye umri wa miaka 78, amekosoa kile anachokiita mazoea katika jeshi, akisema kuwa maafisa wengine wakuu wanazingatia zaidi utofauti, usawa, na kujumuishwa kwa jinsia zote kuliko utayari.
Sasa, Trump, akiwa nyuma ya Biden kuchukua madaraka, ana uwezekano wa kubatilisha agizo la Biden na atachukua hatua mbele kwa kuwaondoa wanajeshi wanaohudumu kwa sasa, The Times iliripoti.
a