Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania Trump wamepata maambukizi ya ugonjwa wa Corona. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Trump ameandika “Usiku huu, first lady na mimi tumekutwa na maambukizi ya Covid-19. Tutaanza kujitenga kwa ajili ya matibabu mara moja. Kwa pamoja tutalishinda hili”.
Hii ni baada ya msaidizi wake Hope Hicks kukutwa na ugonjwa huu mapema jana baada ya kusafiri nae katika ndege ya Rais (Air Force One) siku ya Jumanne wakati akielekea jimbo la Cleveland kwenye mdahalo na mpinzani wake Joe Biden.
Daktari wa Trump amesema Rais huyo ataendelea na majukumu yake chini ya uangalizi maalum kipindi chote hicho. Hii sio mara ya kwanza kwa ikulu ya Marekani kupata mgonjwa wa Corona ambapo mwezi May msaidizi wa makamu wa Rais alikutwa na Corona na baadae kupona.