April 1, 2020 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustine Ndugulile amefanya ziara ya kukagua utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Corona katika maeneo mbalimbali ikiwemo vituo vya afya, hospitali na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuwahifadhi wagonjwa watakaobainika mkoani Dodoma.
“Tuendelee kutoa elimu kuhusu namna ya kujikinga na virusi hivi vya Corona, juzi nilitoa elimu kidogo watu wakaelewa kwamba hivi virusi vina ukuta wa mafuta na sabuni inayeyusha mafuta kwahiyo unaponawa maji kwa sabuni na virusi hivyo vinakufa” Ndulile
“Sasa hivi kumekuwa na upotoshaji, kuna mtu jana tena mkubwa sana ananipigia simu ananiambia Waziri nataka kujinyunyilizia maji ya limau na ndimu kwenye pua nimeambiwa inaua virusi nikamuambia wewe unajiletea matatizo makubwa”-Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustine Ndugulile
CORONA MGONJWA APATIKANA DSM, WAWILI WAPONA