Thomas Tuchel amethibitisha kuwa ataondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu, kama ilivyopangwa.
Kulikuwa na ripoti kwamba Mjerumani huyo angesalia kuinoa klabu hiyo, kutokana na ugumu wa Bayern kutafuta mrithi.
Lakini Tuchel anasema yeye na klabu hawakuweza kufikia makubaliano kuhusu yeye kuendelea.
“Tunasalia na makubaliano tuliyokuwa nayo Februari,” Tuchel alisema. “Tulikuwa na mazungumzo kama ilivyoripotiwa katika wiki iliyopita lakini hatukuweza kupata makubaliano, kwa hivyo tunasalia kwenye makubaliano tuliyokuwa nayo Februari.”