Spika wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amesema kuwa atahakikisha taarifa zote sahihi za Bunge hilo zinawafikia wananchi ili isije ikaonekana Bunge hilo halifanyi kazi na halisikiki kwa sababu wabunge wengi waliomo ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Spika Ndugai, ametoa kauli hiyo leo Novemba 10, 2020, mara baada ya kula kiapo cha kuendelea kushika nafasi hiyo, ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuwapa usia wabunge kuwa, wajitahidi kuzungumza na wasiwe mabubu kwa manufaa ya wananchi wao waliowapigia kura.
“Tutajitahidi katika Bunge hili taarifa nyingi za Bunge zinawafikia wananchi, tukijifungia hapa habari zisiwafikie wananchi, Bunge hili litakuwa limehukumiwa toka mwanzo kwa kuwa lina wabunge wengi wa CCM ndiyo maana halisikiki, halifanyi kazi na halionekani, lazima Bunge hili lionekane, lisikike linavyoishauri na kuiambia serikali” Spika Ndugai
LIVE BUNGE: NDUGAI APITA KWA KISHINDO, WABUNGE WAMTAFUTA WAAPISHWE
https://youtu.be/tOhQrW6b0p8