Tume ya ushindani nchini FCC na shirikisho la wenye viwanda tanzania CTI zimesaini mkataba wa mashirikiano ya namna bora ya kubadlishana taarifa hasa kwenye sheria ya ushindani ya alama za bidhaa.
Makabidhiano hayo yamesainiwa jijin Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine wameeleza ushirikiano huu utasaidia viwanda kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi na kuongeza mapato nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa tume ya ushindani William Erio akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utiaji saini amesema wakati rais Samia anaendelea kufungua milango kwenye sekta ya uwekezaji,taasisi zilizo chini ya wizara ya viwanda na biashara zinatakiwa kuwa na mkakati wa kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanaimarishwa.
Nae mkurugenzi mtendaji wa CTI mhandisi Leodard Tenga amesema sekta ya viwanda ina mchango mkubwa katika uzalishaji wa bidhaa mbali mbali ambayo bado amekiri kutofanya vizuri kama ilivyokusudiwa.