Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia ,(ATMIS) imesema Jumapili kuwa imeanza kutoa mafunzo ya siku tano ili kuwapa ujuzi na elimu wafanyakazi wake wa kukabiliana na mahitaji yao ya afya ya akili na saikolojia wakati wanahudumu kwenye tume hiyo.
Mafunzo hayo kuhusu afya ya akili na usaidizi wa kisaikolojia katika shughuli za kusaidia amani yameandaliwa na Ofisi ya Msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia (UNSOS) kwa ushirikiano na Kituo cha Mafunzo ya Kulinda Amani cha Kimataifa cha Kofi Annan chenye makao yake makuu mjini Accra (KAIPTC), na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani ( GIZ).
Mafunzo ya afya ya akili na saikolojia kwenye operesheni za amani yamewaleta pamoja maafisa wa polisi na jeshi ambao wapo kwenye maeneo ya vurugu, vifo na maangamizi, ambapo watajifunza kuhusu namna migogoro inavyoathiri afya ya akili, familia, jamii na matokeo ya kiwewe na sonona wanayopata baada ya walinda amani wa tume hiyo kupata taharuki, na namna ya kusimamia sonona wakati wanatumikia tume hiyo.
Mwakilishi maalumu wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia na mkuu wa ATMIS Mohammed El-Amine Souef wakati akifungua mafunzo hayo ametaja hatari na changamoto za afya ya akili wanazokabiliana nazo walinda amani.
Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kinaendesha mafunzo ya siku tano ili kuwapa wafanyakazi ujuzi na maarifa ya kukabiliana na mahitaji yao ya afya ya akili na kisaikolojia wanapohudumu katika misheni hiyo.
Mwakilishi Maalum wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (SRCC) nchini Somalia, Balozi Mohamed El-Amine Souef, ambaye alizungumza kwenye sherehe za ufunguzi mjini Mogadishu, alielezea hatari na changamoto za afya ya akili zinazowakabili wafanyakazi katika misheni za kulinda amani.
‘Tunakabiliwa na vurugu, vifo na uharibifu, ambayo inaweza kuathiri vibaya hali yetu ya kiakili na kusababisha msongo wa mawazo baada ya kiwewe cha machafuko (PTSD),”
Wakati wa mafunzo, wafanyakazi wa ATMIS watajifunza kuhusu jinsi migogoro mikali inavyoathiri afya ya akili, familia, jamii na athari za kiwewe na mkazo wa baada ya kiwewe [PTSD]kwa walinda amani na misheni na jinsi ya kudhibiti mfadhaiko unapohudumu katika misheni yoyote.