Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole, amewaonya viongozi na wagombea wa nafasi mbalimbali katika chama hicho wajiepushe na siasa za kusema watu badala yake wajikite kufanya siasa zenye kuzingatia ustaarabu.
Amezungumza hayo wakati akitaja majina ya wagombea wa uwakilishi kwa upande wa Zanzibar.
“Tufanye siasa za kistaarabu na sisi tumezindua kampeni juzi vizuri kabisa hatutaki kusema watu, tunasema hoja tunaziwekea sababu na tunaeleza tunachotaka kupeleka kwa watanzania” Polepole